Serengeti Boys yaichapa tena Burundi
Shangwe kwa Vijana maarufu kwa Jina Serengeti Boys baada ya kuibuka Kidedea kwa bao 2-0 kwa kuitandika Burundi (U17) kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba leo.
Timu ya Vijana U17 ya Burudi leo kwenye uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba imepoteza mchezo wake wa pili tena wa kirafiki baada ya kukubali kuchapwa bao 2-0 na Timu ya Serengeti Boys ya jijini Dar es salaam inayojiandaa na safari ya Gabon. Mchezo wake wa kwanza wa kirafiki walinyukwa bao 3-0 na Timu ya Vijana maarufu kwa jina la Serengeti Boys katika uwanja huo huo wa Kaitaba.
Katika mchezo wa leo bao la kwanza lilifungwa na Issa Abdu Makamba dakika ya 36 kipindi cha kwanza jezi namba 6 mgongoni aliyelifunga kwa mpira wa adhabu (frii kiki) na kuzama moja kwa moja. Bao la pili lilifungwa dakika za majeruhi dakika ya 89 na Ibrahim Abdallah na mtanange kumalizika kwa bao 2-0 ikiwa ni jumla ya bao 5-0 ikiwa ni jumla ya mchezo wa kwanza na wa pili. Serengeti sasa baada ya kuvuna ushindi huo mkubwa wanapanda ndege kwenda Jijini Dar es Salaam kucheza na Timu ya U-17 ya Ghana Jumatatu mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.
Category: tanzania
0 comments