Liverpool yaendeleza ubabe wake
Pambano la ligi kuu ya England baina ya wapinzani wa jadi katika jiji la Liverpool kati ya wenyeji Liverpool na Everton limemalizika kwa ushindi kwa Liverpool wa bao 3-1
Liverpool ilifanikiwa kufunga mabao yake kupitia kwa Sadio Mane dakika ya 8 kabla ya Methiew Pennington hajaisawazishia Everton huku Philip Coutinho akifunga bao la pili dakika ya 31 na Divock Origi kumalizia la mwisho dakika ya 60.
Category: uingereza
0 comments