Yanga yarudi kileleni baada ya kuichapa Azam
Mabingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga imepanda kileleni mwa maimamo wa ligi hiyo baadavya kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.
Shujaa wa mchezo huo alikua mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia Obrey Chirwa akifunga bao pekee katika mchezo huo baada ya makosa ya Walinzi wa Azam FC.
Azam FC itawabidi wajilaumu wenyewe kwani kwa muda mwingi walikua wakimiliki mpira huku wakipata nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia.
Yanga sasa imefikisha pointi 56 pointi 1 mbele ya Simba ambao watacheza kesho dhidi ya Kagera Sugar.
Category: tanzania
0 comments