Man United yabanwa mbavu nyumbani
Mashetani wekundu wa Old Trafford klabu ya Manchester United imebanwa nyumbani na kulazimishwa sare ya bila kufungana na wageni West Brom Albion.
Licha ya kutawala kwa kiwango kikubwa katika mchezo wa leo lakini kukosekana kwa Zlatan Ibrahimovic pengine kunaweza kuelezwa kama ni moja ya sababu za kushindwa kupata goli baada ya Zlatan kuongoza katika orodha ya wafungaji bora wa United msimu huu.
Hii ni sare ya 8 nyumbani kwa Manchester United msimu huu na kufanya harakati zao za kutinga katika Top 4 kuzidi kuwa ngumu
United sasa imefikisha pointi 53 katika nafasi ya 5
Category: uingereza
0 comments