Samattah kacheka na nyavu tena Genk
Baada ya kufunga magoli mawili kwenye mchezo wa Europa League wakati Genk ilipocheza ugenini dhidi ya Gent, leo March 12, 2017 Samatta ameendeleza moto wa kutupia kambani kwenye ligi kuu ya Ubelgiji kwa kufunga goli moja wakati timu yake ikipata ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya KVC Westerlo.
Samatta alifungua nyavu za Westerlo mapema tu dakika ya 7 kipindi cha kwanza, magoli mengine ya Genk yakafungwa na Thomas Buffel 27′, Omar Colley 67’na Ruslan Manilovsky 90+2′.
Wafungaji wa magoli matatu ya leo, wote walifunga pia katika mechi ya iliyopita ya Europa League (Samatta, Colley na Manilovsky).
Ushindi huo unaifanya Genk ifikishe jumla ya pointi 48 ikiwa katika nafasi ya nane (8) kwenye msimamo wa ligi ya Ubelgiji inayoshirikisha timu 16.
Category: uingereza
0 comments