Arsenal yalipiza kipigo kombe la FA
Mchezo huo ulikua ni mmoja kati ya michezo miwili ya kombe la FA iliyochezwa leo ukitanguliwa na mechi nyingine baina ya Middlesbrough na Manchester City ambapo Man City waliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-0.
Magoli ya Arsenal leo yalifungwa na Theo Walcot,Olivier Giroud,Alexis Sanchez, Aaron Ramsey na goli la kujifunga la mlinzi wa Lincoln Luke Watfall.
Kwa matokeo hayo sasa Arsenal imeungana na Manchester City kutinga nusu fainali ya michiano hiyo mikongwe kabisa kwa klabu duniani.
Category: uingereza
0 comments