Simba yaipiga Polisi 3-0
SIMBA SC wameendelea kuwapa raha mashabiki wao, baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji Polisi Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo ameendelea kuwatesa makipa wa Tanzania baada ya kufunga bao la kwanza kipindi cha kwanza katika mchezo huo wa kirafiki jioni ya leo.
Dakika 45 za kwanza zilimalizika Simba wakiwa mbele kwa bao 1-0, lakini kipindi cha pili wakaongeza mabao mawili kupitia kwa winga wake machachari Shiza Kichuya kwa penalti na mshambuliaji Juma Luizio.
Kipindi cha pili kocha Mcameroon alifanya mabadiliko ya karibu kikosi chote kutoka wachezaji walioanza kipindi cha kwanza.
Kikosi cha Simba kilikuwa; Peter Manyika, Janvier Bokungu/Hamad Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’/Vincent Costa, Abdi Banda, Juuko Murshid, James Kotei/Moses Kitandu, Muzamil Yassin/Jonas Mkude, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Said Ndemla, Laudit Mavugo/Juma Luizio, Ibrahim Hajib/Pastory Athanas na Shiza Kichuya/Mwinyi Kazimoto
Category: tanzania
0 comments