Habari njema kwa mashabiki wa Ronaldo
Hispania.Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anategemea kuwa baba wa watoto mapacha wa kiume hivi karibuni, ilida chanzo kutoka katika familia yake.
Mama ya watoto hao anayeisha pwani ya magharibi Marekani anamimba kubwa na inasemekana atajifungua hivi karibuni.
Nyota huyo wa Real Madrid (32), aliwaambia watu wake wa karibu kuwa mapacha hao watafikia katika jumba lake kubwa lililojengwa kwa gharama ya pauni 5 milioni katika jiji la Madrid.
Chanzo hicho kilisema: “Cristiano na familia wake wamejianda kuwapokea watoto hao katika familia yao.
“Nyota huyo hataki kuweka wazi maisha yake binafsi, lakini aliwaambia rafiki zake wa karibu kuwa anategemea kupata watoto wa kiume hivi karibuni.”
Ronaldo kwa sasa anamahusiano na mrembo Georgina Rodriguez (23), haijawahi kusemwa kwamba anategemea kupata watoto mapacha.
Hii ni mara ya pili kwa Ronaldo kuficha jina la mwanamke aliyezaanaye kama ilivyokuwa kwa mama wa mtoto wake Cristiano Jr, inasemekana mwanamke huyo alipewa pauni 10 milioni na Mreno huyo kutojitangaza kuwa ni mzazi mwezie.
Category: uingereza
0 comments