Mbwana Samattah hakamatiki

Unknown | 12:40 PM | 0 comments

Siku chache baada ya kuifunga mabao mawili katika ligi kuu ya Ubelgij dhidi ya Club Brudge nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta jana usiku pia alikua mmoja kati ya wachezaji waliozungumzwa sana katika vyombo mbali mbali vya habari akifunga bao 2 kati ya bao 5-2 walizopata Genk dhidi ya wapinzani wao Gent kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya Europa League.

Ikicheza Ugenini Genk iliweza kuibuka na ushindi huo mkubwa ugenini unaowafanya kutanguliza mguu mmoja ndani katika timu zinazowania kucheza hatua ya robo fainali kwani ili itolewe itabidi ikubali kufungwa zaidi ya bao 3-0 katika mechi ya marudiano wiki ijayo.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments