Simba balaa .... Wairarua Yanga bila ya huruma

Unknown | 6:05 AM | 0 comments


Kombe la Mapinduzi limeendelea kuliza mashabiki na wanachama wa Yanga baada ya kukumbana na vipigo viwili mfululizo ndani ya siku 4

Ikiwa haijasahau machungu ya kufungwa bao 4-0 na Wana Lambalamba Azam FC Yanga leo imekubali kichapo kingine toka kwa mahasimu zao katika soka la Tanzania Wekundu wa Msimbazi Simba.

Mchezo huo wa nusu fainali ya pili katika michuano ya kombe la mapinduzi ulimalizika kwa sare ya bila kufungana na ndipo changamoto ya mikwaju ya penati ikatumika kuamua mshindi wa mchezo huo na Simba kufanikiwa kushinda kwa penati 4-2.

Kipa namba moja wa Yanga Deo Munishi na Mlinzi wa pembeni Mwinyi Haji walishindwa kumfunga kipa namba moja wa Simba Daniel Agyei penati zao zikidakwa kwa ufundi na kipa huyo raia wa Ghana.

Simba wao walikosa penati moja kati ya penati walizopiga na aliyekosa ni mlinzi wa kati Method Mwanjale penati yake ikidakwa na Deo Munishi.

Nahodha Jonas Mkude, Kipa Daniel Agyei,Kiungo Mzamiru Yasini na beki wa pembeni Javier Besala Bokungu ndio waliopata penati za Simba.

Kwa matokeo hayo Simba sasa itakutana na Azam katika mchezo wa Fainali siku ya Ijumaa ya tarehe 13 Januari 2017 baada ya Azam kutangulia kutinga fainali katika mechi ya mapema wakiifunga Taifa Jang'ombe.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments