MSN ya Barcelona yarejea na kuivusha Barca
Miezi mitatu ya ukame wa magoli kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil na Barcelona Neymar umefikia mwisho baada ya kufunga goli moja katika ushindi wa bao 3-1 walioupata Barcelona dhidi ya Athletic Bilbao.
Barcelona ilikua ikihitaji ushindi wa zaidi ya bao 3 kuweza kuvuka hatua hii ya 16 bora ya kombe la Mfalme nchini Spain maarufu kama Copa Del Rey baada ya kupoteza bao 2-1 katika mechi ya awali wiki iliyopita.
Ni Usiku ambao muunganiko wa washambuliaji watatu wa Barcelona yani Messi,Suarez na Neymar wote walifunga huku Luis Suarez akitangulia kufunga bao la kwanza kabla ya Neymar hajaongeza la pili kwa njia ya penati
Beki wa kushoto wa Bilbao Enric Saborit alifunga bao moja na kufanya matokeo kuwa 2-1 mpaka dakika ya 77 Lionel Messi alipofunga bao la ushindi kwa njia ya mpira wa adhabu ndogo na Barcelona kutinga sasa Robo fainali.
Category: uingereza
0 comments