Ronaldo ambwaga tena Mesi tuzo ya mchezaji Bora

Unknown | 10:57 AM | 0 comments


Kwa mara nyingine ndani ya mwezi mmoja Cristiano Ronaldo anatangazwa tena kuwa mchezaji bora wa mwaka na safari hii akipata tuzo hiyo toka Shirikisho la Soka Duniani.

Ronaldo ameshinda katika tuzo mpya ya FIFA best player of the year 2016 jijini Zurich Uswiss baada ya kuwabwaga Lionel Messi na Antoine Griezman ambao ndiyo walibaki katika orodha ya wanaowania tuzo hiyo.

Mwezi Uliopita Ronaldo alishinda pia Balon D'or kwa mwaka 2016 akiwabwaga wacheza hao hao yani Messi na Griezman.

Pamoja na tuzo hiyo pia Ronaldo ametajwa miongoni mwa wachezaji 11 bora wa mwaka katika kikosi bora cha mwaka cha FIFA.

Alikabidhiwa tuzo hiyo na Rais wa FIFA Infantino na kuwashukuru wachezaji na bechi la ufundi la Real Madrid na Ureno ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa kkupatiana mafanikio haya.


FIFA THE BEST 2016 AWARD - WASHINDI

Mchezaji bora - Cristiano Ronaldo
Mchezaji bora wanawake  - Carli Lloyd
Kocha bora - Claudio Ranieri
Kocha bora wanawake - Silvia Neid
Uungwana katika soka (Fair Play Award) - Atletico Nacional
Award for Outstanding Career - Falcao
Goli bora la mwaka  - Mohz Faiz Subri
Mashabiki bora  - mashabiki wa Borussia Dortmund na  Liverpool 
Wachezaji 11 bora (FIFAPro World XI ) - Manuel Neuer, Dani Alves, Marcelo, Gerard Pique, Sergio Ramos, Andres Iniesta, Toni Kroos, Luka Modric, Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Luis Suarez 

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments