Simba waendeleza ubabe wa soka
Vinara wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Wekundu wa msimbazi Simba wamehamishia makali yao nje ya Dar baada ya kuibuka na ushindi ugenini katika jiji la Mbeya.
Katika dimba la Sokoine jijini Mbeya wenyeji Mbeya City walikubali kuchapwa bao 2-0 na Simba katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara
Simba iliibukana ushindi huo ikiendeleza wimbi lake la ushindi msimu huu bila kupoteza mchezo wowote mpaka sasa ikiwa ni Raundi ya nane.
Ibrahim Ajib alitangulia kuipatia Simba bao la kwanza kwa mpira wa adhabu ndogo iliyomshinda kipa wa Mbeya City na kuzama kimiani huku Shiza Kichuya akifunga bao la pili baada ya kutumia makosa ya mabeki wa Mbeya City waliokuwa wakimsindikiza.
Fredric Blagnon wa Simba alikosa penati katika pambano hilo baada ya mpira aliopiga kudakwa na kipa wa City.
Kwa matokeo hayo ya bao 2-0 waliyopata Simba leo wanaendelea kushikilia uongozi wa ligi hiyo wakifikisha pointi 20 baada ya kucheza michezo 8
Category: tanzania
0 comments