Yanga yaibamiza Mtibwa 3 - 1

Unknown | 9:10 PM | 0 comments

Mshambuliaji Obrey Chirwa Raia wa Zambia leo amefungua rasmi ukurasa wa magoli ndani ya klabu yake ya Yanga baada ya kufunga moja ya mabao matatu dhidi ya Mtibwa leo.




Yanga iliibuka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Mtibwa mchezo uliopigwa katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam katika mwendelezo wa ligi kuu ya Soka Tanzania bara.

Chirwa alifunga bao la kwanza la Yanga kipindi cha kwanza kabla ya Haruna Chanongo hajasawazisha kwa upande wa Mtibwa huku Simon Msuva na Donald Ngoma nao wakiifungia Yanga jioni ya leo.

Kwa matokeo sasa Yanga wanafikisha pointi 14 katika nafasi ya 4 sawa na Mtibwa wenye pointi hizo pia.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments