Refa aliyecheza mechi ya Simba na Yanga afungiwa

Unknown | 2:09 PM | 0 comments

Habari za kuaminika toka katika kikao cha kamati ya mashindano ya Shirikisho la soka Nchini Tanzania TFF zinaeleza kwamba Mwamuzi Martin Saanya amefungiwa miaka miwili kuchezesha soka.


Hatua hii imekuja baada ya mwamuzi huyo kulalamikiwa kutokana na maamuzi mabovu aliyotoa katika mechi ya watani wa jadi siku ya Jumamosi.

Pamoja na Saanya ambaye alikua ndiye mpuliza kipyenga,balaa hilo la kufungiwa pia limemkuta mwamuzi msaidizi Samwel Mpenzu ambaye alikua mshika kibendera na ni yule ambaye alilalamikiwa kwa kulikataa goli la Simba lililofungwa na Ibrahim Ajib.

Taarifa pia inasema kadi nyekundu aliyopewa nahodha wa Simba Jonas Mkude imefutwa baada ya kamati kujiridhisha kwamba haikua sahihi.

Kinachosubiriwa sasa ni taarifa kamili kutoka TFF kuhusu uamuzi huo.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments