Hawa hapa wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora

Unknown | 2:12 PM | 0 comments

Jumla ya wachezaji watano wamebaki katika kinyang'anyiro cha mchezaji bora wa mwezi Septemba katika ligi kuu ya England.



Na mwezi huo majina yaliyofanikiwa kupenya na walivyovifanya ni hawa hapa

● Kevin De Bruyne (Manchester City)
  Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya Kiungo Amefunga mabao mawili na kusaidia kupatikana mawili kwa mwezi huo

● Adam Lallana (Liverpool)
Amefunga mabao mawili na kusaidia upatikanaji wa mabao mawili.

● Romelu Lukaku (Everton).
Amehusika katika upatikanaji wa mabao mengi zaidi kuliko mchezaji yoyote katika ligi kuu ya England kwa mwezi Septemba.
Akifunga mabao  hat-trick dhidi ya Sunderland, Akiwafunga Crystal Palace na Middlesbrough kila moja bao 1 na kusaidia upatikanaji wa bao moja pia.

● Son Heung-min (Tottenham Hotspur).
Wakati msimu unaanza alikua mmoja kati ya wachezaji ambao ilisemekana watauzwa lakini hali ilibadilika na akabaki kikosini na kwa mwezi wa tisa Amefunga mabao manne, Mawili dhidi ya Stoke City na mawili dhidi ya Middlesbrough.


● Theo Walcott (Arsenal).
Baada ya kurudishwa kucheza kama Winga mchezaji huyu amerudisha pia makali yake na kupenya katika wachezaji bora wa mwezi Septemba akiwa Amefunga mabao mawili na kuiwezesha Arsenal kushinda michezo mitatu mwezi Septemba.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments