Ratiba ya mechi za leo na kesho Ligi kuu Tanzania Bara

Unknown | 12:19 PM | 0 comments

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea leo Oktoba 7, 2016 kwa michezo miwili ambapo Kagera Sugar itaikaribisha Toto Africans kwenye Uwanja Kaitaba mkoani Kagera wakati Stand United itakuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mkesho
Mbali ya mechi hizo za leo, kesho Jumamosi Oktoba 8, 2016 pia kutakuwa na michezo mitatu ambako Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati African Lyon itaikaribisha Ndanda FC jijini Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikiialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi ulioko mkoani Pwani.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments