SISSOKO AJIUNGA TOTTENHAM
Klabu ya Tottenham imefanya juu chini juu kuhakikisha inamsajili mshambuliaji Moussa Sissoko katika hatua za mwisho za usajili kabla ya kufungwa kwa dirisha, usiku wa kuamkia leo.
Spurs imemwaga pauni million 30 kumpata mshambuliaji huyo Mwafrika mwenye asili ya Ufaransa. Na ililazimika kukodi ndege ili kuwahi kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Tayari ametua katika klabu hiyo na kuvaa jezi akionyesha sasa atakuwa jijini London badala ya jijini Newcastle.
Category: uingereza
0 comments