SIMBA, RUVU SHOOTING KUUFUNGUA UWANJA WA UHURU LEO
Nyasi za Uwanja wa Uhuru au Shamba la Bibi kama unavyojulikana na wengi Leo zitazikaribisha Simba watakaokua nyumbani kuwakaribisha wageni wa Ligi hiyo Ruvu Shooting.
Simba na Ruvu Shooting zote zitaingia uwanjani zikiwa na kumbukumbu ya sare katika mechi zao zilizopita.
Katika mchezo mwingine hiyo kesho Yanga itakua ugenini mjini Mtwara kucheza na Ndanda Fc ya huko wakati vinara wa ligi hiyo Azam FC watakua wageni wa Prisons jijini Mbeya.
Category: tanzania
0 comments