ERIKSEN AJIFUNGA TOTTENHAM HADI 2020
Kiungo wa kimataifa wa Denmark anayeichezea Tottenham Hotspurs Christian Eriksen ameongeza mkataba wa kuichezea klabu hiyo ya London.
Eriksen amesaini mkataba mpya wa miaka minne wa kuichezea Spurs ambapo sasa atadumu katika klabu hiyo mpaka mwaka 2020.
Hii ni habari njema kwa Tottenham ambayo wiki ijayo itaanza kampeni ya kuwania taji la mabingwa barani Ulaya.
Category: uingereza
0 comments