Serengeti Boys yaifumua Kongo 3 - 2
Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuibanjua Congo kwa bao 3-2Mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za vijana ulikua ni wa kwanza kwa timu hizo kabla ya kurudiana wiki mbili zijazo nchini Congo Brazaville ambapo bingwa wa jumla atafuzu.
Serengeti Boys ikicheza katika dimba la taifa lililojaa watazamaji waliokua wakishangilia muda wote ilitandaza soka safi na kuibuka na ushindi huo.
Magoli ya Mashujaa hao wa Taifa yalifungwa na Yohana Costa aliyefunga mabao mawili peke yake huku bao moja likifungwa Issa Abdi na kuifanya timu hiyo kuhitaji sare au ushindi wowote katika mechi ya marudiano ili kufuzu.
Category: tanzania
0 comments