Man United wachapwa na Watford 3 - 1

Unknown | 5:17 PM | 0 comments

Hali imezidi kuwa mbaya kwa Manchester United baada ya kupoteza mchezo wake wa 3 mfululizo baada ya kukubali kichapo cha bao 3-1 toka kwa Watford.



Wakisafiri mpaka katika uwanja wa Vicarage Road Man United wamekubali kichapo hicho kwa magoli ya Etienne Capoue, Juan Zuniga na Troy Deneey huku Marcus Rashford akifunga bao pekee la United.

Matokeo hayo yameendeleza hali ya Sintofahamu kwa kikosi cha Jose Mourinho baada ya kuonekana si lolote si chochote licha ya pesa nyingi zilizotumika katika usajili ikibaki na pointi zake 9 baada ya michezo mitano.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments