Real Madrid yavunja rekodi ya Barca La Liga

Unknown | 2:51 PM | 0 comments


Real Madrid wamecharaza Espanyol 2-0 na kufikia rekodi ya Barcelona ya kushinda mechi 16 mfululizo katika ligi kuu ya Uhispania, La Liga.

Ushindi wao mechi hiyo ya Jumapili umewaweka alama tatu mbele kileleni mwa ligi hiyo.

Mabao kutoka kwa James Rodriguez na Karim Benzema yaliwawezesha kufikia rekodi hiyo iliyowekwa na Barcelona walipokuwa chini ya Pep Guardiola msimu wa 2010-11.

Real, walicheza bila nyota wao Gareth Bale na Cristiano Ronaldo ugenini uwanja wa Cornella-El Prat lakini hilo halikuwazuia kuandikisha ushindi wao wa nne kutoka kwa mechi nne walizocheza msimu huu.
Rodriguez amefunga mabao mengi kutoka nje ya eneo la hatari kushinda kiungo mwingine yeyote wa kati ligi tano kuu za Ulaya tangu 2014-15

Barcelona wanashikilia nafasi ya pili ligini kwa sasa wakiwa na alama tisa, sawa na Las Palmas. Madrid wana alama 12.

Klabu 10 zinazoongoza La Liga

Klabu Mechi Mabao Alama

1 Real Madrid 4 9 12

2 Barcelona 4 8 9

3 Las Palmas 4 6 9

4 Atl Madrid 4 9 8

5 Sevilla        4 3 8

6 Villarreal   4 3 8

7 Eibar       4 1 7

8Sporting Gijón 4 -3 7


9 Ath Bilbao 4 0 6
10 Alavés       3 1 5

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments