RAIS MPYA WA UEFA HUYU HAPA ....

Unknown | 1:51 PM | 0 comments

Akiwa na miaka 48 tu Aleksander Ceferin amechaguliwa kiwa Rais mpya wa Shirikisho la soka Barani Ulaya Uefa..


Ceferin anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Michael Platini aliyelazimishwa kujiuzulu baada ya kashfa ya matumizi mabaya ya pesa ndani ya shirikisho la Mpira duniani hali iliyopelekea yeye na Rais wa FIFA aliyepita Sep Blatter kufungiwa miaka 8 kujihusisha na soka.

Ceferin ambaye ni rais wa shirikisho la soka nchini Slovenia amepata kura 42 dhidi ya 13 za mpinzani wake Michael Van Praag raia wa Uholanzi.

Ceferin ambaye ana elimu ya sheria amekua Rais wa soka nchini Slovenia tangu mwaka 2011 na sasa atahudumu kama Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya mpaka mwaka 2019.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments