Matokeo yote kamili ya mechi za jana za UCL
Mechi za mwisho za hatua ya kwanza ya makundi katika ligi ya mabingwa barani Ulaya zimekamilishwa usiku huu kwa mechi 9 kuchezwa.
Sergio Aguero aliibuka shujaa katika ushindi wa bao 4-0 walioupata Manchester City dhidi ya Wajerumani Borussia Monchengledbach.
Aguero alifunga hat-trick katika mchezo huo ikiwa ni siku moja tu tangu Lionel Messi alipofanya hivyo pia katika ushindi wa bao 7-0 walioupata Barcelona dhidi ya Celtic huku bao la moja likifungwa na Kelechi Iheanacho.
Mechi hiyo ni kiporo cha mechi ya kundi C iliyoshindwa kufanyika Jumanne kutokana na mvua kubwa jijini Manchester.
Huko Ubelgiji wenyeji Club Bruge walikumbana na kichapo cha bao 3-0 toka kwa Mabingwa wa ligi kuu ya England Leicester City magoli mawili ya Ryad Mahrez na moja la Marc Albrighton.
Mechi hiyo ya kundi G iliambatana na mechi nyingine baina ya FC Porto ya Ureno na FC Kobenhavn ya Denmark mechi iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mabingwa watetezi Real Madrid wao wakiwa nyumbani iliwabidi kupigana na kupata ushindi dakika za mwisho ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Sporting Lisbon. Cristiano Ronaldo na Alvaro Morata wakifunga bao 1 kila mmoja.
Mechi nyingine ya kundi hilo F ilishuhudia Borussia Dortmund wakiibuka na ushindi mnono wa bao 6-0 wakiwafunga Legia Warsaw hao Legia wakiwa nyumbani kwao Poland.
Katika dimba la Wembley ambalo Tottenham Hotspurs wanalitumia kama uwanja wa nyumbani kwao kupisha matengenezo ya uwanja wa White Hart Lane walikubali kufungwa bao 2-1 toka kwa Monaco ya Ufaransa.
Mechi hiyo ya kundi E iliambatana na mechi ya Bayer Leverkusen na CSKA Moscow mechi iliyomalizika kwa sare ya bao 2-2.
Katika Kundi H Juventus ambao ni mabingwa wa Italia wakiwa nyumbani walilazimishwa sare ya bila kufungana na Sevilla ya Spain.
Olimpic Lyon ambao nao wako katika kundi hilo H waliifunga Dinamo Zagreb bao 3-0.
Category: uingereza
0 comments