JOSE MOURINHO AENDELEZA UBABE .... AIBUKA KOCHA BORA
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho ametangazwa kuwa kocha bora wa mwezi Agosti katika ligi kuu ya England.
Mourinho ameiongoza Man United kushinda mechi zote 4 katika mwezi Agosti.
Man United walianza mwezi huo kwa kuwashinda Leicester City bao 2-1 katika ngao ya jamii,Wakaifunga Bournemouth 3-1 katika mechi ya Ufunguzi wa ligi kuu,wakashinda 2-0 dhidi ya Southampton Old Trafford kabla ya kumaliza mwezi kwa kuifunga Hull City bao 1-0 ugenini.
United ni kati ya timu 3 ambazo zimeshinda mechi zake zote za ligi nyingine ni Manchester City na Chelsea.
Category: uingereza
0 comments