HAWA HAPA MAKOCHA WANAOWANIA TUZO YA KOCHA BORA WA MWEZI
Mchakato wa Tuzo ya kwanza ya kocha bora wa mwezi Agosti katika ligi kuu ya England kwa msimu mpya wa mwaka 2016/2017 unaendelea.
Jose Mourinho kocha wa Manchester United,Pep Guadiola kocha wa Manchester City,Antonio Conte wa Chelsea na Mike Phelan wa Hull City ni majina ya makocha wanne ambao wanawania tuzo ya kocha bora wa mwezi Agosti.
Ni Phelan pekee ambaye amepoteza mchezo mmoja mpaka sasa lakini Conte Mourinho na Guadiola wote wameibuka na ushindi katika mechi zao 3 walizocheza mwezi Agosti.
Category: uingereza
0 comments