MAN U YAIPIGA KAMOJA HULL CITY

Unknown | 6:32 AM | 0 comments


Goli la dakika za mwisho la mshambuliaji chipukizi wa Manchester United Marcus Rashford ndilo lililoipa Manchester United Ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Hull City.


Hull City inayofundishwa na kocha msaidizi wa msaidizi Manchester United Mike Phelan ilionekana kuimarika vilivyo katika mchezo huo wakicheza kwa uangalifu na kutofanya makosa.

Mpaka dakika 90 United ilishindwa kupata bao lolote lakini juhudi binafsi za nahodha Wayne Rooney zilizaa bao safi lililofungwa na Marcus Rashford ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Juan Mata.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments