ARSENAL WAANZA KUTAKATA
Hatimaye Arsenal wamepata ushindi wao wa kwanza msimu huu wakiifunga Watford bao 3-1 ugenini.
Arsenal ambayo ilianza kwa kichapo toka kwa Liverpool kisha ikatoka sare na Leicester City imeweza kujikwamua na kupata ushindi huo kwa magoli ya Santi Carzola,Mesuit Ozil na Alexis Sanchez.
Katika mchezo mwingine mabingwa watetezi Leicester City waliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Swansea magoli ya Jarmie Vardy na nahodha Wes Morgan
Chelsea wao waliendeleza wimbi la ushindi kwa kuinyuka Barnley bao 3-0 magoli ya Eden Hazard,Willian na Victor Moses.
MATOKEO YA MECHI ZA LEO EPL
- Tottenham 1-1 Liverpool
- Watford 1-3 Arsenal
- Leicester City 1-2 Swansea
- Chelsea 3-0 Burnley
- Southampton 1-1 Sunderland
- Everton 1-0 Stoke
- Crystal Palace 1-1 Bournemouth
Category: uingereza
0 comments