YUSUPH MANJI AMETOA MAAGIZO MAZITO YANGA

Unknown | 10:21 PM | 0 comments

MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Mehboob Manji ametoa agizo kwamba asisajiliwe mchezaji yeyote kutoka Uganda au Kenya hata awe mzuri kama Cristiano Ronaldo.
Kisa? Manji amewaambia viongozi wenzake wa Yanga na benchi la Ufundi kwamba wachezaji wa Kenya na Uganda ni wasumbufu hivyo hataki kuona wanasajiliwa.
Badala yake sasa, Manji ametaka wasajiliwe wachezaji kutoka Afrika Magharibi na kwingine na kwa sasa klabu hiyo ipo katika mchakato wa kuleta kiungo kutoka Niger.
Kiungo wa kimataifa wa Niger, Issoufou Boubacar Garba anatarajiwa kuwasili leo usiku kwa majaribio ya wiki moja kabla ya kocha Hans van der Pluijm kutoa uamuzi.

Issoufou Boubacar Garba anatarajiwa kuwasili leo kwa majaribio Yanga SC


Dirisha dogo la usajili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara linafungwa Desemba 15 na kweli Mholanzi, Pluijm aliyempendekeza mchezaji huyo atakuwa na wiki moja tu ya kutoa majibu juu ya Mniger huyo aliyezaliwa Februari 2, mwaka 1990.

Taarifa zinasema Garba kwa sasa anacheza kwao baada ya kuondoka Tunisia ambako alisajiliwa na klabu za Club Africain na ES Hammam-Sousse lakini akawa hapati nafasi ya kucheza, ingawa mwenyewe anadai kwa hila na visa si sababu ya uwezo.

Popote katika wasifu wake, Garba anatambulishwa kama kiungo – lakini Yanga wanasema wanaleta mshambuliaji.

Na huyu atakuwa mchezaji wa pili kuletwa na kocha Pluijm, baada ya awali kumleta beki Joseph Zuttah ambaye hata hivyo aliachwa baada ya mechi saba.

Garba aliyezaliwa mji wa Niamey, mwenye urefu wa futi 5 na inchi 6, kisoka alianzia klabu ya AS FAN ya kwao mwaka 2010, kabla ya kuhamia Thailand ambako alichezea klabu za Muangthong United mwaka 2011 na Phuket.

Mwaka 2012 alitua Club Africain ya Tunisia ambako hakucheza mechi hadi anahamishiwa 

ES Hammam-Sousse ambako pia hakucheza.

wasifu wake unaonyesha tangu ameondoka ES Hammam-Sousse hajapata timu nyingine, lakini uongozi wa Yanga SC umejiridhisha anachezea klabu bingwa ya kwao, AS Douanes.

BIN ZUBERY BLOG

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments