SANCHEZ ATWAA TUZO ENGLAND
MSHAMBULIAJI
Alexis Sanchez amewashinda Jamie Vardy, Sergio Aguero na Harry Kane na
kunyakua tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Mashabiki England.
Mpachika
mabao huyo wa Arsenal pia amewashinda kipa wa Manchester United, David
De Gea na nyota wa Everton, John Stones kutwaa tuzo hiyo ambayo mwaka
2013 ilichukuliwa na Luis Suarez na 2014 Aguero.
Mchezaji
huyo wa kimataifa wa Chile mwenye umri wa miaka 26 kwa sasa yuko nje
kwa maumivu ya nyama za paja ambayo yatamchukua wiki nne kuanza kurejea
uwanjani na leo alipokelewa tuzo hiyo na kocha wake, Arsene Wenger
ambaye atamkabidhi baadaye usiku huu.
Kocha Arsene Wenger akiwa amempokelea tuzo Alexis Sanchez ambayo atamkabidhi baadaye usiku huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Category: uingereza
0 comments