AFARIKI UWANJANI AKICHEZA MECHI

Unknown | 10:18 PM | 0 comments


KIUNGO wa zamani wa Kano Pillars, Abdul Haruna (pichani kushoto) amefariki dunia jana wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya Kano Professionals na kikosi cha wachezaji wateule wa Kano.
Taarifa zinasema kwamba Haruna alianguka wakati wa mchezo kabla ya kufariki dunia.

Mabingwa hao wa zamani wa Nigeria, 
Kano Pillars, wameandika katika ukurasa wao wa Twitter habari za kifo cha mchezaji wao huyo wa zamani.
“Tunasikitika kutangaza kifo cha Abdul Haruna. Nafsi yake ipumzishwe kwa amani. Amin,” wameandika Pillars.

Bobsam Elejiko, Amir Angwe, Endurance Idahor, Samuel Okwaraji na Emmanuel Ogoli ni baadhi ya wachezaji wa Nigeria walioanguka uwanjani na kupoteza fahamu awali, kabla ya kufariki dunia.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments