JOHN TERRY AREJEA MAZOEZINI CHELSEA
NAHODHA
wa Chelsea, John Terry amerejea mazoezini na kumpa matumaini mapya
kocha Jose Mourinho kuelekea mchezo muhimu wa Kundi G Ligi ya Mabingwa
Ulaya Jumatano dhidi ya Porto.
Terry,
ambaye anafikisha miaka 35 leo, amekaribishwa tena mazoezini sambamba
na kiungo Mbrazil, Ramires katika mazoezi ya asubuhi leo Uwanja wa
Cobham uliopo makao makuu ya The Blues.
Na
anaweza kuingia moja kwa moja kwenye kikosi ambacho kinahitaji angalau
pointi moja Uwanja wa Stamford Bridge kujihakikishia kuingia hatua ya 16
Bora ya Ligi ya Mabingwa.
Terry alifanya mazoezi mapema wiki
iliyopita, lakini akaonekana hayuko fiti kiasi cha kutosha kucheza mechi
dhidi ya Bournemouth Jumamosi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Sasa
mshambuliaji 'aliyechuja' Radamel Falcao ndiye anabaki mchezaji pekee
anayekosekana Chelsea kutokana na mchezaji huyo wa zamani wa Manchester
United kuwa bado anasumbuliwa na maumivu ya misuli.
Terry
amekosa mechi mbili zilizopita za Chelsea – Jumamosi wakifungwa 1-0 na
Bournemouth na katika sare ya 0-0 na Tottenham – kutokana na kuumia
kifundo cha mguu katika mchezo dhidi ya Maccabi Tel Aviv mwezi uliopita.
Alifanya mazoezi mapema wiki iliyopita, lakini akaonekana hayuko tayari
kuanza kucheza.
Category: uingereza
0 comments