Messi akiri Ronaldo ni noma

Unknown | 4:13 PM | 0 comments

Messi ameulizwa kuhusu tofauti yake na Ronaldo ambapo Messi amesema yeye na Ronaldo wako poa tu akini kila mtu anajaribu kupambana ili kuonesha alichonacho uwanjani ila nje ya uwanja hakuna tofauti kati ya nyota hao wawili.

Kuhusu uwezo wa Ronaldo uwanjani Lioneil Messi amesema Ronaldo ni “bora sana” alisema “tunajaribu kufanya kitu bora kwa ajili ya timu zetu kila mwaka lakini kuhusu nje ya uwanja sifikirii sana kama hilo ni muhimu,dunia nzima inajua kuhusu Ronaldo ni mcheza bora na ndio maana ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani.”

Lakini pia Messi alizungumzia taarifa za kuongeza mkataba mpya ndani ya Barcelona ambao utaisha mwaka 2021 akisisitiza ya kwamba hana mpango wa kuondoka Nou Camp na anataka kumalizia maisha yake ya soka katika uwanja huo kwani hilo ndiop jambo ambalo amekuwa akiliota kila siku.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments