Yanga yatwaa ubingwa
Kama Ulivyosikia ndivyo ilivyotokea kwa mara nyingine tena katika Historia ya Ligi kuu Soka Tanzania Bara,Mabingwa Watetezi Yanga wanatwaa kwa mara nyingine ubingwa wa ligi kuu msimu huu kwa kuwafunga Toto Africans ya Mwanza.
Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 jioni hii katika dimba la Taifa jijini katika mchezo ambao kuna baadhi ya wadau wa Soka walikua wakidhani pengine Yanga wangewaachia Toto Africans ili kuwanusuru na janga la kushuka daraja linalowakabili.
Amiss Tambwe ameingia katika vitabu vya kumbukumbuku ya ubingwa wa Yanga msimu huu akifunga bao pekee kwa kichwa dakika ya 82 ya mchezo bao ambalo liliwanyima raha kabisa Toto ambao walionekana kuwabana vyema Yanga dakika zote za mchezo.
Kwa Matokeo haya Yanga wanafikisha pointi 68 huku wakiwa na mtaji mkubwa wa magoli ya kufunga na kufungwa tofauti ya magoli 44 wakiwa wamebakiza mechi moja sawa a wapinzani wao Simba na njia pekee ya Yanga kuzuiwa ubingwa huu ni kufungwa katika mechi ya mwisho kwa idadi kubwa ya magoli pia Simba washinde kwa magoli zaidi ya 12-0 jambo ambalo linaonekana kama ni kitendawili.
Kazi kubwa sasa wanayo Toto Africans na inawezekana kabisa wakashuka daraja baada ya mechi ya Mwisho kwani mpaka sasa wana pointi 29 nafasi ya pili toka mkiani mwa Msimamo wa ligi.
Category: tanzania
0 comments