Goli 3 Pointi 3 zilivyoirudisha Simba SC kileleni ligi juu Tanzania Bara

Unknown | 10:01 AM | 0 comments


Wekundu wa msimbazi Simba wameendelea kugawa dozi katika mechi zake za ligi kuu ikiibuka tena na ushindi wa bao 3-0 baada ya kupata ushindi kama huo katika mechi iliyopita wakiifunga Majimaji ya Songea.

Simba imeweza kuibuka na ushindi huo leo kwa kuifunga Prisons ya Mbeya katika mchezo uliopigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba ilitawala vilivyo mchezo huo hasa dakika za mwanzo za kipindi cha kwanza  na kufanikiwa kupata bao mapema tu dakika ya 18 likifungwa na Juma Luizio baada ya juhudi kubwa za beki Bokungu aliyeamua kupanda na kupiga krosi iliyotua katika kichwa cha Novart Lufunga ambaye alimtengenezea mfungaji.

Dakika ya 38 Laudit Mavugo alimtengenezea vyema Ibrahim Ajibu ambaye aliupiga kiufundi na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Simba ikiwa mbele kwa ushindi wa bao 2-0

Kipindi cha pili kilikua ni cha kumalizia tu kwa Simba na dakika ya 68 Ibrahim Ajibu aliambaa na mpira katika winga na kupiga krosi iliyotua katika kichwa cha Laudit Mavugo aliyefunga bao hilo la tatu.

Kwa matokeo hayo Simba sasa inafikisha pointi 51 na kure

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments