Barcelona yapangwa na Atlentico Madrid nusu fainali .... Ratiba kamili ya Copa Del Rey hii hapa ...

Unknown | 10:18 AM | 0 comments

Ratiba ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Mfalme nchini Spain maarufu kama Copa Del Rey imepangwa leo asubuhi.


Mabingwa watetezi Barcelona watakua na wakati mgumu kutetea ubingwa wao baada ya kupangwa kucheza dhidi ya Atletico Madrid katika hatua ya nusu fainali.

Barcelona ambao wametinga hatua hiyo baada ya kuwatupa nje Real Sociedad kwa kuwafunga jumla ya magoli 6-2 watakutana na Atletico Madrid ambao wao wametinga hatua ya nusu fainali kwa kuwatoa Eibar kwa ushindi wa jumla wa magoli 5-2.

Mechi nyingine ya Nusu fainali itakua Celta Vigo ambao wameitoa Real Madrid hatua ya robo fainali watacheza dhidi ya Alaves.

Ratiba ya mechi za nusu fainali ya kwanza inaonyesha timu hizo zitakutana Februari 1 ambapo Celta Vigo wataanzia nyumbani sawa na Atletico Madrid na marudiano ni wiki moja badae tarehe 8 Februari 2017.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments