Hali tete Yanga

Unknown | 8:56 PM | 0 comments

Taarifa nyingine ambayo imetufikia inasema kocha msaidizi Juma Mwambusi ataendelea kukinoa kikosi cha Yanga mpaka kocha mpya atakapoanza kazi November 1. Endelea kuifuatilia wapendasoka.com

******************************


Kwa mujibu wa Meneja Hafidh Saleh, si kweli kwamba benchi zima la ufundi limejiuzulu, yeye binafsi hajaandika barua ya kujiuzulu wala hajapata taarifa yoyote kutoka kwa uongozi wa Yanga.

"Siyo kweli, hizo ni taarifa za kupikwa na mimi nazisikia tu kwenye vyombo vya habari kwamba eti sisi tumepeleka barua za kujiuzulu"

"Mimi na kocha Mwambusi tupo kazini tunajiandaa na mechi ya keshokutwa na hatujapata taarifa yoyote kutoka kwa uongozi"


*******************************

Anayetajwa kuchukua nafasi ya meneja ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo Sekilojo Chambua, japo mwenyewe amekana kupokea taarifa yoyote.

********************************


Taarifa iliyotufikia hivi punde inasema kocha wa Yanga Hans Van Der Pluijm amejiuzuru rasmi kuifundisha timu hiyo

Kumekuwa na taarifa za ujio wa kocha mpya George Lwandamina kutoka Zambia ambaye alifika nchini jana  lakini viongozi wa Yanga wamekua wakizikanusha na kusisitiza kwamba  Pluijm baso ni kocha wao japo taarifa ya uhakika ni kwamba

Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema tayari barua ya Pluijm imepokelewa na uongozi umeridhia kujiuzulu kwake.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments