MCHEZAJI MKONGWE AFARIKI DUNIA .... TFF WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Unknown | 9:35 PM | 0 comments



Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Morogoro inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, John Mabula(Mwenye jenzi ya njano)

Mbali ya Mtibwa Sugar, taarifa za Mabula ambaye pia amewahi kuchezea Moro United ya Morogoro na Shinyanga Shooting ya Shinyanya kwa mafanikio nafasi ya ulinzi kwa muda mrefu katika timu hizo, aliuawa kwa kuchomwa kisu na mwenzake alipokuwa akiamulia ugomvi huko Kitunda - nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Rais Jamal Malinzi amemwelezea Mabula kuwa ni mchezaji aliyekuwa na uwezo na uadilifu na mchango wake katika soka utabaki katika dhana ya kumbukumbu ya wachezaji mahiri wa Tanzania waliotokea kucheza nafasi ya ulinzi japokuwa ametangulia mbele za haki.

Rais Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa uongozi wa timu ambazo alicheza ambazo ni Mtibwa Sugar, Moro United na Shinyanga Shooting; kadhalika familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki walioguswa na msiba huo wa gwiji huyo aliyepata pia kucheza timu ya taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ ya mwaka 2002-2004.

Rais Malinzi amewaasa wadau wote kuwa watulivu wakati huu mgumu wa msiba wa mpendwa wetu Mabula hasa kutokana na mazingira ya kifo. Bwana ametoa, Bwana Ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. Amina.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments