SIMBA, AZAM ZAIFAIDISHA YANGA

Unknown | 7:41 PM | 0 comments

Matokeo ya sare kati ya Simba dhidi ya Azam yanaifaidisha Yanga ambayo imeendelea kukaa kileleni mwa ligi bila presha kubwa kutoka kwa Simba na Azam ambazo zimeshindwa kupata matokeo ya ushindi ili kuisogelea Yanga kileleni.

Timu zote zilishindwa kutumia nafasi kadhaa ambazo zilitengenezwa katika mchezo huo lakini Hamisi Mcha atajilaumu mwenyewe kwa kushindwa kuipa goli Azam dakika ya anane alipo baki yeye na golikipa wa Simba lakini shuti lake dhaifu liliishia mikononi mwa Vicent Agban.

Haji Ugando, Emiry Nimubona, wote walipata nafasi kwa upande wa Simba lakini hawakuweza kuzibadili kuwa magoli.

Mchezo huo ulikuwa muhimu kwa timu zote mbili kutokana na nafasi zao katika ligi, kama Azam ingeshinda mchezo wa leo ingefikisha pointi 61 pointi 4 nyuma ya Yanga lakini kama Simba ingeshinda ingefikisha pointi 60 na kuwa nyuma ya Yanga kwa pointi tano. Matokeo ya leo yanaifanya Yanga kujitanua kileleni kwa kuizidi Azam pointi 6 nyuma ya Yanga huku Simba ikiwa nyuma ya watani zao kwa pointi 7.

Timu hizo tatu ambazo zilipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa VPL msimu huu zimebakiza mechi 4 baada ya kucheza mechi 26 hadi sasa huku Simba ikiwa nyuma kwa gap kubwa la pointi ambalo kimahesababu tayari wameshajitoa kwenye kinyang’anyiro cha ubingwa.

Mambo muhimu unayotakiwa kuyafahamu

Azam na Simba hakuna timu iliyopata ushindi zilipokutana zenyewe kwa zenyewe msimu huu. Mchezo wa raundi ya kwanza zilitoka 2-2 na leo wametoka draw (0-0).
Mara ya Mwisho Simba kuifunga Azam ilikuwa May 2, 2015 ilipopata ushindi wa magoli 2-1.
Ushindi wa mwisho wa Azam dhidi ya Simba ilikuwa ni March 30, 2014 ambao ilifanikiwa kuifunga kwa magoli 2-1.
Ramadhani Singano amecheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Simba tangu alipojiunga na Azam mara baada ya kuachana kwa malumbano na klabu yake ya zamani aliyoitumikia tangu akiwa timu ya vijana.
Kwa upande wa Simba, Brian Majwega alikuwa anakipiga dhidi ya timu yake zamani (Azam FC) ambayo alikuwa anaitumikia kabla ya kuingia kwenye mgogoro na kutimkia mtaa wa Msimbazi.
Kocha mkuu wa Simba Jackson Mayanja aliendelea kukosekana kwenye benchi la ufundi baada kutolewa na mwamuzi kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Toto Africans juma lililopita.
Simba imeshindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa tatu mfululizo kwenye mashindano yote (VPL na FC Cup) ilifungwa 2-1 na Coastal Union, ikapoteza tena kwa goli 1-0 dhidi ya Toto kabla ya kubanwa leo na kulazimishwa sare na Azam FC.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments