MBWANA SAMATTA AZIDI KUPAA, ATINGA EUROPA LEAGUE

Unknown | 11:17 AM | 0 comments

Wakati timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Kenya bila ya nahodha wake Mbwana Samatta na kulazimishwa sare ya goli 1-1, Samatta allikuwa uwanjani nae akipambana kuhakikisha klabu yake ya KRC Genk inashiriki Europa League msimu wa 2016/2017.
KRC Genk imefanikiwa rasmi kupata nafasi ya kucheza Europa League msimu wa 2016/2017 baada ya kufanikiwa kuifunga Charleroi kwa jumla ya goli 5-1, Genk walianza kupata goli la uongozi kwa penati kupitia Nikolaos Karelis aliyefunga hat-trick dakika ya 20, 56 na 71 lakiniMbwana Samatta akafanikiwa kufunga goli dakika ya 27 kabla ya Sandy Walshkufunga goli la tatu dakika ya 45.
gnk-cha-jpg_1464529519
Goli pekee la Charleroi lilifungwa na Jeremy Perbet dakika ya 40 ya mchezo, kwa matokeo hayo KRC Genkinayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta watacheza michuano ya Europa League msimu wa 2016/2017 pamoja na vilabu vya Man United na Southampton, hiyo itakuwa ni fursa nyingine kwaSamatta kuonekana.
KRC Genk wataanzia katika hatua ya mtoano na kama watafuzu ndio watapangwa katika hatua ya Makundi yaEuropa League, makundi ambayo yatachezeshwa droo hivyo inaweza ikatokea bahati Kwa KRC Genk yaSamatta kupangwa hata na klabu kubwa kama Man United endapo itafuzu mechi yake ya mtoano.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments