LIONEL MESSI ALAMBA TUZO NYINGINE

Unknown | 3:17 PM | 0 comments

Mshambuliaji wa Klabu Barcelona Lionel Messi amefanikiwa kuchukua Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Januari La Liga baada kufanikiwa kufunga magoli 6 katika mechi 5 alizocheza kwenye ligi hiyo katika huu mwezi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Muargentina huyo kuchukua tuzo hiyo iliyoanzishwa msimu wa 2013/2014.

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameshinda taji hilo mara mbili tangu lianzishwe mnamo mwezi Septemba 2013.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments