Hawa ni maofisa wengine wa FIFA waliokumbwa na kashfa ya rushwa…

Bado hali si shwari ndani ya Shirikisho la soka la mpira wa miguu
duniani FIFA, baada ya kusimamishwa kwa aliyekuwa Rais wa shirikisho
hilo Sepp Blatter na viongozi wengine, headlines zimerudi tena!!.
Kuna maofisa kutoka Shirikisho hilo wamekamatwa na askari kutokana na msako uliofanywa asubuhi ya leo kwenye moja ya hoteli ya Baur Au Lac, huko Zurich, Uswis, wakihofiwa kupanga njama za kupokea rushwa ndani ya Hotel hiyo.
FIFA imethibitisha kuwa, Makamu wa rais, Alfredo Hawit kutoka Honduras na Juan Angel Napout wa Paraguay ni moja ya maafisa waliokamatwa na hii ni mara ya pili sasa kwa maafisa hao kutumia Hotel hiyo kama sehemu ya makutano.
FIFA wamesema
wataendelea kufuatilia kwa kushirikiana na Marekani, kufanya uchunguzi
wa kina ambao unaendeshwa na Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Uswis, kama
ambavyo inakubalika na sheria ya Uswis na kwa sasa haitazungumza lolote
juu ya tukio hilo mpaka uchunguzi utakapokamilika.
Kuna maofisa kutoka Shirikisho hilo wamekamatwa na askari kutokana na msako uliofanywa asubuhi ya leo kwenye moja ya hoteli ya Baur Au Lac, huko Zurich, Uswis, wakihofiwa kupanga njama za kupokea rushwa ndani ya Hotel hiyo.
FIFA imethibitisha kuwa, Makamu wa rais, Alfredo Hawit kutoka Honduras na Juan Angel Napout wa Paraguay ni moja ya maafisa waliokamatwa na hii ni mara ya pili sasa kwa maafisa hao kutumia Hotel hiyo kama sehemu ya makutano.

Alfredo Hawit (aliyekaa katikati) ni mmoja kati ya Makamu wa rais wa FIFA, aliyekamatwa kwenye hotel hiyo.
Category: uingereza
0 comments