VARDY MCHEZAJI BORA WA MWEZI LIGI KUU ENGLAND, WENGER KOCHA BORA
MSHAMBULIAJI
chipukizi wa England, Jamie Vardy amekuwa mchezaji wa kwanza wa
Leicester City kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya
England kwa miaka 15.
Vardy ametwaa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao matano katika mechi nne za Leicester City za Ligi Kuu ya England mwezi uliopita.
Kipa
wa zamani wa England, Tim Flowers alikuwa mchezaji wa mwisho wa
Leicester City kutwaa tuzo hiyo Septemba mwaka 2000 baada ya kufungwa
mabao mawili tu na kuiweka kileleni timu hiyo kwa kukusanya pointi 16
katika mechi nane, wakati chini ya kocha Peter Taylor.
Kocha
Mfaransa wa Arsenal, Arsene Wenger ametwaa tuzo ya Kocha Bora wa mwezi
baada ya kuiongoza timu hiyo kukabana koo na Manchester City kileleni
katika Ligi Kuu ya England.
Category: uingereza
0 comments