MBWANA SAMATTA AIBEBA TP MAZEMBE.
Nyota
wa Tanzania na timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta amefunga goli
moja kwenye ushindi wa magoli 2-0 iliyoupata timu yake ya TP Mazembe
kwenye mchezo wa marudiano wa fainali ya vilabu bingwa Afrika dhidi ya
USM Alger mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Stade TP Mazembe Lubumbashi,
Congo DR.
Ushindi
huo umeifanya TP Mazembe ichukue kombe la vilabu bingwa barani Afrika
kwa mara ya tano lakini ikiwa ni mara ya kwanza kwa wachezaji wa
kimataifa wa Tanzania wanaokipiga kwenye klabu hiyo Mbwana Samatta na
Thomas Ulimwengu.
Samatta
na Ulimwengu wameweka rekodi ya kuwa watanzania wa kwanza kunyanyua
kombe la klabu bingwa barani Afrika huku nyota wengine waliong’ara
zamani kwenye medani ya soka wakishindwa kufanya hivyo.
Mazembe ilishachukua kombe hilo mwaka 1967, 1968, 2009, 2010 na mwaka huu 2015 imefanya hivyo.
Kipindi
cha kwanza cha mchezo huo hakikua na mashambulizi mengi kwa timu zote
mbili hasa kwa upande wa TP Mazembe ambao walionekana kama wanalinda
ushindi wao walioupata kwenye mechi ya awali nchini Algeria. Kipindi cha
kwanza kilimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Kipindi
cha pili Mazembe walianza kusaka ushindi na wakafanikiwa kupata goli la
kuongonza lililofungwa na Mbwana Samatta kwa mkwaju wa penati dakika ya
75 baada ya Roger Assale kuangushwa na beki wa USM Alger akiwa kwenye
eneo la hatari.
Goli
hilo limemfanya Samatta kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo kwa
kufikisha jumla ya magoli nane na kumpiku Bakry ‘Al Medina’ Babiker wa
Al Merreikh ambaye wamekua wakichuana kwa muda mrefu.
Wakati
dakika zikiwa zinaelekea ukingoni Mbwana Samatta alitengeneza goli
jingine ambalo lilifungwa na Roger Assale ambalo lilimaliza kabisa ndoto
za USM Alger kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza.
TP
Mazembe wamekuwa mabingwa kwa jumla ya magoli 4-1 dhidi ya USM Alger,
mchezo wa fainali ya kwanza uliochezwa Algiers, Algeria ulimalizika kwa
Mazembe kushinda kwa magoli 2-1 huku mchezo wa marudiano ambao umepigwa
jijini Lubumbashi, Congo DR ukimalizika kwa TP Mazembe kushinda kwa
magoli 2-0.
Ubingwa
huo unawapa Mazembe tiketi ya kushiriki fainali za vilabu bingwa
duniani zitakazofanyika December mwaka huu nchini Japan.
TP
Mazembe inaungana na mabingwa wa Ulaya Barcelona na mabingwa wa Copa
Libertadores River Plate ambao tayari wamejihakikishia nafasi kwenye
fainali hizo huku mabingwa wa Oceania klabu ya Auckland City pamoja na
mabingwa wa Amerika Kusini Club America wakiwa tarari kwenye orodha
hiyo.
Bingwa
wa Asia kati ya Al-Ahli au Guangzhou Evergrande Taobao na J-League
wataungana wataungana na vilabu vingine na kufanya jumla ya vilabu nane
vitakavyocuana kwenye fainali hizo.
Category: tanzania
0 comments