Lionel Messi amekubali kujiunga na klabu ya Arsenal ila kwa sharti hili …

Unknown | 8:13 AM | 0 comments




Staa wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi November 16 ameingia katika headlines baada ya stori zake za kutaka kujiunga na Arsenal kuandikwa katika headlines za magazeti ya Ulaya, awali Lionel Messi ambaye ameichezea FC Barcelona toka akiwa mdogo aliwahi kukiri kuvutiwa kujiunga na klabu ya Arsenal ya Uingereza.

Messi-490728

Messi ambaye wengi wamewahi kumkejeli na kudhani kuwa hana uwezo wa kutamba nje ya FC Barcelona anatajwa kuwa radhi kujiunga na Arsenal ila sharti lake la mshahara ndio tatizo linalotajwa kuwa huenda hana lengo la kwenda Arsenal, Messi anatajwa kuiomba Arsenal iwe inamlipa mshahara wa pound 600000/= kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 1 za Tanzania mshahara ambao ni mgumu kwa Arsenal kumlipa hususani kwa hulka za kocha wa timu hiyo.

hi-res-2b2f4449796e8b2e48790d5220f12f0d_crop_north

Stori za Lionel Messi kuvutiwa kujiunga na Arsenal aliwahi kukiri kupenda kuichezea klabu hiyo ila November 16 habari zinazotajwa kuwa za kichunguzi kutoka katika gazeti la Star Sport zinasema Messi ameombwa kulipwa mshahara kiasi ambacho ni kigumu kwa Arsenal kukubali au kumudu kulipa, Lionel Messi kwa sasa anatajwa kulipwa mshahara usiofikia pound 300000/= kwa wiki na FC Barcelona na kwa upande wa Arsenal mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa ni Mesut Ozil pound 140000/= kwa wiki.

CT4my_cWwAESlOf

U

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments