Jina la mgombea mwingine wa Urais FIFA limeondolewa kwenye orodha
Uchaguzi mkuu wa Shirikisho la soka
duniani unatarajiwa kufanyika Februari 26, 2016 na tayari viongozi
mbalimbali wamejitokeza kuwania nafasi ya Urais iliyokuwa ikishikiliwa
na Sepp Blatter.
Musa Bility raia
wa Liberia ni mmoja wa wanachama waliojitokeza kuwania nafasi hiyo
lakini jina lake limeondolewa kutoka kwenye kinyang’anyiro hicho kwa
sababu za kimaadili.
Mpaka sasa Shirikisho hilo linalosimamia soka duniani limeidhinisha wagombea watano tu huku Rais wa UEFA Michel Platini naye pia hajajumuishwa kwenye orodha hiyo ya wagombea.Waliopitishwa kuwania nafasi hiyo ni Mwana wa mfalme Ali bin al-Hussein, Jerome Champagne, Gianni Infantino, Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa na Tokyo Sexwale.
Fifa imesema haitazungumzia zaidi sababu za kutemwa kwa Bility, ambaye amepanga kupinga uamuzi huo katika mahakama ya kutatua mizozo ya michezo na imeamua kutotoa maelezo zaidi kuhusu sababu hizo kwa maslahi ya Bility.
Kwa sasa Bility ndiye rais wa chama cha soka Liberia.
Sepp Blatter kwa sasa amesimamishwa kazi na anachunguzwa kwa tuhuma za ufisadi na nafasi yake imezibwa na Issa Hayatou kutoka Cameroon.
Category: uingereza
0 comments