Baada ya Mohamed Dewji kuweka wazi lengo lake la kutaka kuinunua klabu ya Simba, huu ndio mtazamo wa Aden Rage…
Wiki kadhaa nyuma mfanyabiashara mkubwa na maarufu Tanzania Mohamed Dewji aliweka wazi dhamira yake ya kutaka kuinunua klabu ya Simba na kuwekeza bilioni 20 kwa ajili ya klabu hiyo, Dewji lengo lake ni kununua hisa asilimia 51 za klabu ya Simba na kuiwezesha ifike mbali.
Taarifa za Dewji
kutaka kuinunua klabu hiyo zilitoka wiki kadhaa nyuma na kuthibitisha
kuwa tayari ameeleza dhamira ya lengo lake hilo kwa Rais wa sasa wa
klabu ya Simba Evans Aveva na kumwambia aandike barua rasmi ya kuomba kuuziwa klabu hiyo, Stori za November 4 mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo Ismail Aden Rage ameeleza mtazamo wake kuhusu wazo la Mohamed Dewji, vipi kama angekuwa yeye ndio Rais angefanyaje?
“Tatizo
ni kwamba wanachama wetu sisi wanapenda tu vilabu vyao na mashabiki
wanapenda kuchangia michango yao kwa kulipa viingilio uwanjani ila
tatizo ni kwamba vilabu vyetu havipati udhamini wa maana ila usidhani
kama mtu mmoja pekee anaweza kufanya mabadiliko katika mpira hakuna
duniani mafanikio kama hayo”>>> Aden Rage
“Kama
ningekuwa Rais wa Simba kwa sasa kuhusu suala la mtu kumiliki hisa
nyingi katika klabu kwanza ningefanya utafiti wa kuangalia Hispania
wanafanya nini, Ujerumani wanafanya namna gani,baada ya hapo
ningelipeleka kwa wanachama kwa sababu ile klabu sio ya
kwangu”>>> Aden Rage
Category: tanzania
0 comments