YANGA YACHINJA MNYAMA TAIFA .... YAIPIGA VIWILI TU
YANGA YALIPA KISASI, ‘YAUA MNYAMA’ DIMBA LA TAIFAKlabu ya Yanga leo imewapa raha wapenzi na mashabiki wake hii leo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya watani wao wa jadi Simba SC katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo ambao timu zote mbili zilionesha dhamira ya ushindi, Simba iliyotawala zaidi kipindi cha kwanza, ilishindwa kutumia nafasi kadhaa ilizoweza kutengeza ikiwemo ile aliyopata Said Ndemla dakika za mwisho huku Yanga wakiweza kutumia nafasi chache walizopata kukwamisha mipira miwili wavuni.
Golikipa wa Yanga Ally Mustapha Bahtez aliweza kuonesha kiwango cha hali ya juu kwa kupangua michomo kadhaa ya hatari kutoka kwa washambuliaji wa Simba wakiwemo Awadh Juma, Hamisi Kiiza na Mussa Hassan ‘Mgosi’
Katika mchezo huo pia, beki wa Yanga Mbuyu Twitte alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi ya pili ya manjano dakika ya 90.
Kwa ushindi huu Yanga imelipiza kisasi kwani katika mchezo uliopita Simba ikiwa haipewi nafasi, iliweza kuishinda Yanga kwa bao 1-0 lililofungwa na Emmanuel Okwi.
Yanga sasa imefikisha pointi 12 ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja, huku Simba ikibaki na point zake 9 kwa kushinda mechi 3.
Category: tanzania
0 comments