YANGA FC YAITWANGA AZAM FC NA KUTWAA NGAO YA JAMII
Yanga yaendeleza ubabe wake wa kutwaa ngao ya jamii kwa kuitwanga Azam FC kwa mikwaju 8 kwa 7 ambapo Kelvin Yondan amepeleka kilio kwa Azam.
Bao pekee la Salum Telela mwaka 2013 liliipa Yanga SC ushindi wa Ngao, wakati mwaka jana, mabao mawili ya Mbrazil Genilson Santana Santos ‘Jaja’ na moja la Simon Msuva yaliipa tena timu hiyo taji hilo.
Yanga SC hadi sasa ndiyo timu iliyotwaa mara nyingi zaidi Ngao ya Jamii, kuanzia mwaka 2001 ikiifunga 2-1 Simba na 2010 ikiwafunga tena watani wao hao kwa penalti 3-1 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika ya 90 na mwaka juzi na mwaka jana ikiifunga Azam FC.
Inafuatia Simba SC iliyotwaa Ngao mara mbili, 2011 wakiifunga Yanga SC 2-0 na 2012 wakiifunga Azam FC 3-2, wakati Mtibwa Sugar ni timu nyingine iliyowahi kutwaa Ngao mwaka 2009 ikiifunga 1-0 Yanga SC.
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana Julai 29, mwaka huu Azam FC ilishinda kwa penalti 5-3 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Na mchezo wa leo pia unaweza kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti, iwapo timu hizo zitamaliza dakika 90 kwa sare. Hakutarajiwi kuwa na mabadiliko makubwa kutoka vikosi vilivyokutana mara ya mwisho katika Kagame.
Ingizo jipya upande wa Yanga SC inayofundishwa na Mholanzi, Hans van der Pluijm wanatarajiwa kuwa beki Mtogo, Vincent Bossou, kiungo Mzimbabwe Thabani Kamusoko na mshambuliaji Matheo Simon ambao walisajiliwa baada ya Kagame.
Upande wa Azam FC inayofundishwa na Muingereza, Stewart John Hall itaendelea kumkosa mshambuliaji mpya, Mkenya Alan Wanga iliyemsajili Julai kutoka El Merreikh ya Sudan, ambaye amechelewa kuungana na wenzake kutokana na msiba wa mama yake mzazi.
Brian Majwega na majeruhi Kipre Balou pia wanatarajiwa kuendelea kukosekana, lakini Ramadhani Singano ‘Messi’ yuko fiti na kuhusu kuanza mbele ya Farid Mussa aliyeng’ara Kombe la Kagame, Stewart ataamua.
Na ikumbukwe Azam FC inaingia katika mchezo wa leo, ikitoka kushinda mechi 13 mfululizo chini ya kocha Hall, ikiwa imefungwa mabao mawili tu katika mechi ya kwanza kabisa dhidi ya Friends Rangers Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Baada ya hapo, nyavu za Azam FC hazijaguswa tena kuanzia kwenye mechi za kirafiki hadi Kombe la Kagame na hizi tatu za kirafiki Zanzibar- jumla mechi 12 makipa wa Azam FC ‘hawajalokota kunyavu’.
Ukuta wa Yanga SC umekuwa ukiruhusu mabao karibu katika kila mechi na hivi karibuni katika mechi zake za kujipima kwenye kambi ya Mbeya, ilifungwa mabao matatu katika mechi tatu, ikishinda 3-2 dhidi ya Mbeya City 3-2, 4-1 dhidi ya Kemondo na 2-0 dhidi ya Prisons.
Mshambuliaji wa Yanga SC, Donald Ngoma akitaafuta maarifa ya kumtoka beki wa Azam FC, Abdallah Kheri timu hizo zilipokutana mwezi uliopita katika Robo Fainali ya Kagame |
VIKOSI VYA LEO VINATARAJIWA KUWA:
Azam FC:
Aishi Manula, Shomari Kapombe, Agrey Morris, Abdallah Kheri, Paschal
Wawa, Jean Mugiraneza, Himid Mao, Frank Domayo, Farid Mussa, John Bocco
na Kipre Tchetche.
BENCHI; Mwadini Ali, Said Mourad, Erasto Nyoni, David Mwantika, Salum Abubakar, Ame Ally, Ramadhani Singano, Didier Kabumbangu na Mudathir Yahya.
Yanga SC: Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Mwinyi Mngwali, Kevin Yondani, Nadir Haroub, Thabani Kamusoko, Deus Kaseke, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amisi Tambwe na Godfrey Mwashiuya.
BENCHI; Mudathir Khamis, Juma Abdul, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Vincent Bossou, Salum Telela, Metheo Simon, Malimi Busungu, Simon Msuva na Said Juma.
BENCHI; Mwadini Ali, Said Mourad, Erasto Nyoni, David Mwantika, Salum Abubakar, Ame Ally, Ramadhani Singano, Didier Kabumbangu na Mudathir Yahya.
Yanga SC: Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Mwinyi Mngwali, Kevin Yondani, Nadir Haroub, Thabani Kamusoko, Deus Kaseke, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amisi Tambwe na Godfrey Mwashiuya.
BENCHI; Mudathir Khamis, Juma Abdul, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Vincent Bossou, Salum Telela, Metheo Simon, Malimi Busungu, Simon Msuva na Said Juma.
Farid Mussa akimtoka beki wa Yanga SC, Juma Abdul katika Robo Fainali ya Kagame mwezi uliopita
Credit: Bin Zubeiry
|
Category: tanzania
0 comments